Top Stories

RC Shigela awahimiza Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kujikita katika shughuli Ujasiriamali

on

Mkuu wa mkoa Morogoro Martine Shigela amewataka wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe pamoja na vyuo vingine mkoani humo kujikita katika ujasiriamali pindi wawapo chuoni ili kukiingizia kipato.

RC Shigella ametoa wito huo wakati akifungua kongamano la ujasirimali lilofanyika chuo kikuu Mzumbe ambalo Linafahamika kama Mzumbe day ambapo amesema wapo baadhi ya wanafunzi wanamawazo ya kizamani ya kutegemea mikopo pekee badala ya kufanya shuguli zingine.

.

Aidha Shigela ameongeza kwa kusema Serikali inasisitiza jamii kujikita katika shughuli hizo kutokana na mfumo wa ajira wa Sasa kwani wasomi wamekua wengi tofauti na zamani.

” sisi wakati tunasoma tukimaliza tunapangiwa ajira siku hiyo hiyo unachagua mwemywe lakini kwa Sasa idadi ya wasomi imeongezeka hivyo ajira za Serikali ni chache lazima wanafunzi wajiongeze “

Katika hatua nyingine RC Shigella amepongeza chuo Cha Mzumbe kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya Ujasirimali Jambo ambalo linazalisha wasomi wenye weredi na maarifa makubwa katika utendaji kazi.

Shigela amevitaka vyuo vingine binafsi na Serikali Mkoani humo kukga mfano huo kwani unaondoa malalamiko ya ajira kwa Serikali.

Awali ,Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lugano kusiluka amesema progamu hiyo imeanza mwaka 2017 na inafanyika Kila mwaka huku lengo likiwa kuongeza hamasa kwa wanafunzi kuwa na moyo wa kujiajiri badala ya kusubiria ajira za Serikali.

.

Profesa Kusiluka anasema tangu kuanza kwa kongamano Hilo wajasiriamali zaidi ya 150 wamenufaika kwa kupata elimu na kufungua viwanda vidogo ambayo wametoa ajira kwa vijana wenzao.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi ambao wamenufaika na kongamano la ujasirimali Oshaidi Mtegama Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya amesema kwa Sasa anategeneza majiko yanayotumia chenga za mkaa na upepo ambao unazalisha nishati ya umeme nakutumika.katika kupika

Anasema baada ya kuhitimu masomo yake hategemei kuajiriwa hivyo anawasihi wanafunzi wengine kujichanganya na jamii ili kupata ujuzi

 

Tupia Comments