Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego ameamua kutumia kipaji chake cha Sanaa kwa kuimba nyimbo ya msanii Mbilia Bel inayoitwa Nakei Nairobi kwa kumchangia walemavu wa Ngozi wa familia moja yaani mama na mtoto na kufanikiwa kupata kiasi cha shilingi laki mbili na 20 kwenye kongamano la fursa na biashara lililofanyika mkoani Singida
“wapo kina mama wenzetu wenye matatizo ya ulemavu wa Ngozi na mnajua shida wanayoipata kwenye jua, shida wanayoipata kwenye mafuta lakini kuna mwingine yeye na mtoto wote wana changamoto hiyo kwa hiyo mimi nimetumia mdomo wangu na naomba nimkabidhi hizi hapa laki mbili na elfu 20 ukanunue mafuta ya mtoto wetu mzuri, mzungu mzuri kweli kweli si ndio ”
Aidha Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dengego amemuagiza stahiki meya na mkurugenzi wa halmashauri wa manispaa ya Singida kuhakikisha hadi June mwaka huu wawe wametoa mikopo ya 10% kwa wajasiriamali waliokidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo.
Kauli hiyo ameitoa katika kongamano la biashara na fursa lililofanyika mkoani Singida ambapo amefanikiwac kukabidhi hundi ya shilingi bili 1.1 ambazo zinatakiwa kutolewa hadi mwezi juni
“Niwapongeze manispaa tunaenda kutoa mkopo ya million 168 lakini ndani yake tuna billion 1.1 hela hizi n zenu vijana , hela hizi ni zenu wanawake na hela hizi ni zenu ndugu zetu wenye ulemavu nah ii hela yote itoke kaqbla ya mwezi wa sita mwaka huuu”