Mkuu wa Mkoa wa Tanga OMARY MGUMBA amewataka Viongozi na wadau wa Elimu kujitahidi kuweka mikakati ya kuongeza Ufaulu kwa kupambana na viashiria vinavyopelekea kutofanya Vizuri kwenye mitiani ya kitaifa ikiwemo ukatili, Mimba za utotoni,ajira kwa watoto ikiwemo ya upatikanaji wa Chakula mashuleni.
Ametoa maelekezo hayo wakati akiongea na wadau wa Elimu Mkoa wa Tanga katika kilele cha siku ya wadau wa Elimu ngazi ya Mkoa kikiwa na malengo Kufanya tadhimi nakupanga mikakati ya kuongeza Ufaulu wakiwemo Maafisa,elimu,wakuu wa Elimu, Viongozi wa siasa na mashirika na Wanafunzi kwenye kilele cha juma la Elimu mkoani Tanga.
“Miongoni mwa changamoto tulizo nanzo ni mdondogo wa wanafunzi ya ni wanafunzi wanaanza wengi lakwanza lakini wakifika darasa la pili wana kuwa wachache na hadi wakifika darasa la saba wanakuwa wachache zaidia hivyo naelekeza kwa wakurugenzi wote kufatilia na kutoa taarifa kila mwezi ya maudhurio ya wananfunzi ili kufahamu changamoto inayo endelea na kutafutia ufumbuzi” Alisema RC Mgumba
Aidha afisa elimu wamkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi alisema kuwa kunachangamoto nyingi zinazopelekea Ufaulu kuwa wa chini kwenye maeneo yetu moja ni kupungua kwa kasi ya ufatiliaji swala la elimu ni moja ya sababu inayo shusha kabisa ushukaji wa Ufaulu wa Elimu huku jambo lengine likiwa ni swala la utoro wa Wanafunzi pamoja na wazazi kushindwa kufatilia maendeleo ya watoto wao.