on air with millardayo

EXCLUSIVE: Rachel Kizunguzungu amrudia Mungu… ni baada ya yote aliyofanya na kupitia

on

Mwimbaji Rachel ambaye ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kujiunga na nyumba ya vipaji Tanzania (THT) na kuanza kuachia nyimbo zake, amekaa kwenye Excluvie na mtangazaji wa Amplifaya ya CloudsFM Millard Ayo na kueleza kilichotokea mpaka akakwama na kukaa kwenye nchi ya watu kwa zaidi ya miezi saba, ishu yake ya kuvuta bangi na mengine.

KUHUSU KUMRUDIA MUNGU: Ni kweli nimemrudia Mungu, ni maamuzi ambayo nimeyafanya mwenyewe baada ya kuona vitu ni vilevile, dunia ni ileile na watu ni walewale ndio maana nikaona sio vibaya nikaja na upande mwingine lakini hii haimaanishi kwamba nitakua nafanya muziki wa Injini, nitaendelea na bongofleva lakini muda mwingi nitautumia kanisani.

KUHUSU OMAN: ‘Ni kweli nimekaa nchini Oman kwa zaidi ya miezi saba, nilikwenda kwa ajili ya kufanya shows tu lakini nikapata tatizo kwenye VISA yangu, nilifanya show za kuandaa mwenyewe ikafanikiwa mwanzoni lakini baadae hali ikabadilika, nilikua na VISA ya miezi mitatu na nikaenda kwenye wiki za mwisho’

Rachel 6

‘Niliamua kuongeza VISA ili nibaki Oman, nikatoa pesa mtu anilipie lakini kumbe hakwenda kulipia… nikakaa nikawa nadaiwa pesa nyingi maana unachajiwa kwa siku pale unapoongeza siku bila VISA, nikawa sitoki kwenda nje kutembea najifungia tu ndani kwa miezi yote, nyumbani watu wakapanic napigiwa simu Mama kalazwa hospitali sababu yangu…. ila baadae ndio nimekuja kupata pesa nikalipa faini nikarudi Tanzania’

KUOLEWA NA MUARABU OMAN: ‘Waswahili wanaoishi Oman hawapendani, hawapendi maendeleo ya watu, wana majungu na wakawa wananitafutia ugomvi nigombane nipigane Polisi, kuhusu kuolewa sijaolewa…. naapa sijaolewa, watu waliongea hivyo sababu nilikua na boyfriend ambaye ni Mauarabu, mpaka sasa niko naye… tulikua karibu sana ndio maana watu wakahisi nimeolewa nae

Rachel 2

KUHUSU KUVUTA UNGA: ‘Nimekua nikiona taarifa kwamba mimi natumia dawa za kulevya, nimesikitika sana na ilitokea mara ya kwanza nilikua na msanii mwenzangu kwenye show sijui anatumia hivyo vitu kwahiyo watu wakaona tumeshaungana ila sio kweli, sijawahi hata kuona, najua dada yangu Ray C katokea huko na aliyoyapitia’

KUHUSU KUVUTA BANGI:Kweli nilikua navuta bangi ila sasa hivi nimeshaacha baada ya kukalishwa chini na familia hata boss, nilikua navuta bangi kutokea nilipotoa wimbo wangu wa pili, nilivuta sababu ya stress…. kuna kipindi nilikua natafuta hata mtu wa kunitungia nyimbo, show zilikata na marafiki zangu walikimbia wote kipindi hicho nilipoandikwa kwamba navuta dawa za kulevya

KUHUSU NYIMBO MPYA: ‘Nitatoa single mpya kwenye wiki mbili hizi, tokea niko Muscat natumiwa msg Rachel tumekumiss karibu…. namshukuru Mungu maana msanii kukaa nje kwa miezi alafu watu wakawa wanakumiss hivyo ni bahati… watu wakae karibu tu naachia single mpya soon’

ULIIKOSA YA CHINI BENZ KUKIRI KUHITAJI MSAADA NA UTUMIAJI DAWA ZA KULEVYA? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI..

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments