Leo Jan 26 2016 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekutana na madereva wa TAXI Dar es salaam na amesikiliza kwa umakini malalamiko yao wakidai mfumo wa usafirishaji wa Teknolojia ya kisasa (UBBER) unawaharibia biashara.
Baada ya Mkuu wa mkoa kusikiliza malalamiko yote hayo akawaambia yafuatayo >>> ‘Niwaombe mkakae alafu Alhamisi ijayo viongozi wachache mje na mapendekezo yanayoweza kujibu shauku na matamanio yangu na baadhi ya Wananchi, ninachotaka tuondoke kwenye biashara ya kukadiriana’
‘Tunakadiriana sisi abiria na mwisho wa siku pia tunakadiriwa na TRA sasa nataka abiria wasikadiriwe bali wajue gharama, nataka TRA isiwakadirie bali ijue haki zake kwenu….‘
‘Mawazo yangu niliyonayo, nataka Dar es salaam yote TAXI zote ziwe za UBBER au TAXI mnazopaki nyie au mtu yeyote aliyesajiliwa, aanze kutumia mashine zitakazoonyesha umbali wa safari anayokwenda… ni ili tuue na huu mzizi mwingine wa fitna’ – Paul Makonda
‘Utatuambia wewe unapigaje elfu 20 wakati wenzako tunachoma mafuta kwa gharama hii? manake kama wakitaka nao wataingia kwenye mfumo huu, na sio swala la kutaka…. nikishaamua mie na nyinyi ndugu zangu mkishalielewa tunaliweka kwenye utaratibu, ndani yake tutapata unafuu na wale wanaotumia TAXI Bubu tutawaondoa‘ – Paul Makonda
UNAWEZA KUTAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI KUJIONEA ZAIDI
UBBER ni Teknolojia ya APP kwenye simu inayokuwezesha kupata usafiri wa Taxi kwa kuiita yoyote iliyokaribu na popote ulipo na unaweza kuona picha halisi ya gari na Dereva mwenyewe baada tu ya kumuita.
App hii ambayo imekua ikitumika sana kwenye mataifa mbalimbali inaruhusu Mtu yeyote mwenye gari lake kuwa Ubber, hautahitajika kulipiga mstari gari lako ili lionekane ni TAXI na ni gari lolote linaweza kuwa Ubber iwe ni Rav 4 ama Range Rover, Hiace au IST…
Kampuni hii haimiliki gari hata moja bali inatumia watu wenye magari yao na kuingia makubaliano, kuwapa mfumo huo wa Teknolojia alafu inachukua sehemu ya mapato yanayopatikana.