Habari za Mastaa

Soudy Brown amemhoji Shilole baada ya kudaiwa kuachanisha Ndoa (U heard)

on

August 3, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ameinasa hii inayomuhusu Mwimbaji wa Bongofleva Shilole kudaiwa kusababisha kuachanisha ndoa ya mtu.

Mwanamke anayedaiwa kufanyiwa kitendo hicho amesema kuwa Shilole amesababisha apewe talaka ili apate nafasi ya kufunga ndoa na mwanaume huyo amabaye kwa mujibu wa mwanamke huyo alikuwa mumewe tangu 2014 lakini kwa sasa amemuacha kwa talaka mbili.

>>>”Mke wa pili si huyo Shishi mimi mke wake halali Shilole bado hajamuoa. Tulifunga ndoa 2014, baada ya kumpata huyo Shilole amenipa talaka. Mtoto namuhudimia kwa shida kaniambia Shilole kamwambia anipe talaka, amenipa mbili.” – Husna

Soudy Brown baada ya kupokea malalamiko ya mwanamke huyo aliamua kumpigia simu Shilole ilikupata uhakika wa hili.

>>>“Bwana Soudy niacheni hayo mambo siyataki kabisa, yanawahusu wenyewe wapambane na hali yao wasije kusema mimi nimesababisha, mambo ya Kiswahili sipendi kabisa.” – Shilole

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story

Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ naye amezungumza kuhusu hali ya Jini Kabula

Soma na hizi

Tupia Comments