Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi ametoa ufafanuzi wa taarifa zilizosambaa kwamba amehusika na uamuzi wa Daktari ambaye ni Mganga mkuu wa Singida vijijini kuacha kazi baada ya kumuweka rumande.
Mkuu wa mkoa ameelezea kisa kizima na ninamnukuu ‘Sihusiki na kuacha kwake kazi, nilimuweka ndani November 26 2016 kipindupindu kiliibuka Singida na nikiwa Njombe, yeye akanyamaza….. lakini inawezekana alikua ana haki ya kunyamaza sababu taratibu zinasema ni mpaka kuwe kuna kesi 5 za Kipindupindu‘
‘Kesi ya 5 ilipatikana tarehe 4 December 2016 hakutangaza, amekuja kutangaza na ni baada ya kufatiliwa tarehe 16 ndio fununu zikasambaa kwamba kuna kipindupindu wakati huo wamekufa watu wawili kutokana na kipindupindu‘
‘Nilimuweka ndani kwasababu hakuwa sawasawa, niliona kabisa kabisa yule fikra na mawazo yake na maadili yake hayakua kazini……. nilimuweka ndani masaa 6 na baada ya muda nilimwambia RPC amwachilie aende afanye kazi’ – RC Dr. Rehema Nchimbi.
Mganga mkuu huyo mwenyewe amesema ‘Mkuu wa mkoa alisema nimechelewa kutoa taarifa kitu ambacho sio sahihi kwasababu nisingeweza kutoa taarifa kama sijathibitisha kama ni ugonjwa wa kipindupindu ama la, nimeacha kazi sababu aliona siwezi kufanya hiyo kazi nikaona nikae tu pembeni… huu ni mwaka wa 10 kama Daktari, nitatafuta tu kazi sehemu nyingine‘
KUSIKILIZA KILA ALICHOSEMA MKUU WA MKOA NA DAKTARI HUYO BONYEZA PLAY HAPA CHINI