Leo February 2, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa taarifa ya uchunguzi wake kuhusu biashara ya dawa za kulevya kwenye jiji la Dar es salaam na kuwataja Askari Polisi 9 wanaotuhumiwa kuhusika au kujihusisha na wafanyabiashara wa dawa hizo.
Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo Wamiliki wake wamepewa vibali vya kufanya biashara lakini wanatumia maeneo hayo kinyume na masharti ya biashara kwa kuuza dawa ya kulevya ambapo amewataka kufika kituo kikuu cha polisi kesho saa tano na wasipofanya hivyo atawafata mwenyewe.
'Dar es salaam imekuwa ni lango la kupita na kupeleka madawa ya kulevya'- RC Makonda
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
'Tumekesha usiku tukifutilia biashara hii ya madawa ya kulevya tumekuta inafanyika hadharani'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
'Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua Mungu ataniuliza, niko tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
Mkuu wa mkoa wa DSM, Paul Makonda amewataja askari wasiopungua tisa ambao wanatuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya pic.twitter.com/15SQSGVzVE
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
'Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata'-Makonda pic.twitter.com/xGglHXZqfN
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
'Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya DSM natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe-RC Makonda pic.twitter.com/JgSRaqxyQy
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
'Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya DSM maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
'Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya' RC Makonda pic.twitter.com/B9c73mw2yB
— millardayo (@millardayo) February 2, 2017
RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi pic.twitter.com/Pfnev44pcz