Ni Septemba 13, 2022 ambapo RC Makalla amesema Operesheni ya Panya road ni endelevu wananchi wasiwe na hofu waendelee kufanya shughuli zao za kujiletea kipato kwa kuwa Dar es Salaam ni Salama kabisa, amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa kuhamasisha Ulinzi Shirikishi Katika maeneo yao.
Aidha RC Makalla ameelekeza Magereza yote DSM kuhakikisha Watuhumiwa wa Ujambazi na Panya road Wanapotoka Magerezani taarifa na majina yao ipelekwe kwa OCD au RPC ili kuweza kufuatilia mienendo yao wanapokuwa uraiani.
Sambamba na hilo Mhe Makalla amepongeza ushiriki wa wanachi katika Ujenzi wa Kituo cha Polisi ambapo amesema amejifunza wananchi wakishirikishwa wanaweza kituo hicho ni cha kisasa, cha mfano wananchi maeneo mengine waige mfano huo.
Mradi wa Kituo hicho cha Polisi Mwanagati kukamilika kwake kutagharimu Tsh Milioni 211,964,400 mpaka kituo kilipofikia sasa tayari kimegharimu Tsh Milioni 151,534,400 kati ya hizo shilingi milioni 45,000,000 ni mchango wa Halmashauri, milioni 96,334,400 mchango wa Wananchi na shilingi milioni 10,200,000 mchango wa Serikali Kuu ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Hata hivyo RC Makalla amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kupata kiasi cha milioni 60 ambacho kinahitajika kukamilisha Ujenzi wa Kituo, huku akiagiza kufikia ijumaa awe kupatiwa BOQ ili kujua vifaa vinavyohitajika kwa ili Ofisi yake iweze kusaidia kupitia Wadau wa maendeleo.
Mwisho RC Makalla amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua msingi mkubwa wa maendeleo katika Jamii ni Utulivu ambao unatokana na Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao hivyo DSM ni Salama Serikali ya Mkoa iko makini kusimamia jambo hilo bila kuchoka muda wote usiku na mchana