Michezo

Real Madrid waomboleza kifo cha Kobe Bryant

on

Staa wa Real Madrid Sergio Ramos leo ameingia na jezi ya timu ya taifa ya kikapu ya Marekani yenye jina la Kobe Bryant na namba 10 kama ishara kuomboleza kifo cha staa wa NBA na Los Angeles Lakers Kobe Bryant.

Bryant na mtoto wake Gianna Maria-Onore walifariki jana kwenye ajali ya helicopter ambayo ilipoteza mawasiliano na kuanguka, taarifa rasmi zikatolewa kuwa hakuna aliyesalimika katika ajali hiyo iliyohusisha jumla ya watu tisa.

Real Madrid leo wakiwa na kocha wao Zidane kabla ya kuanza mazoezi walisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha Bryant, huku Ramos akiwa amevaa jezi ya Bryant katika mazoezi hayo kama ishara ya kuomboleza kifo hicho kilichowagusa wengi.

VIDEO: RAHA ILIYOJE !!! BABA MZAZI WA SAMATTA, HAKULALA ANACHEZA MUZIKU UTAMBULISHO WA ASTON VILLA

Soma na hizi

Tupia Comments