Michezo

Real Sociedad waipasua kichwa FC Barcelona

on

Club ya FC Barcelona kwa sasa ina wakati mgumu kufuatia kuumia kwa mshambuiaji wao Ousmane Dembele ambaye amefanyiwa upasuaji na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 6.

Kufuatia kuumia huko FC Barcelona wanataka kumsajili William Jose kutoka Real Sociedad kama ndio mbadala sahihi wa Dembele lakini Real Socoedad wataka dau kubwa ili kuidhinisha dili hilo.

Kocha wa Real Sociedad Imanol ameweka wazi kuwa mchezaji huyo anaweza kuondoka lwa euro milioni 70, kocha huyo inadaiwa katoa kauli hiyo kutokana na kipengele kilichopo katika mkataba wa mchezaji huyo kuwa euro milioni 70 zinaweza kuvunja mkataba wake.

“Kama wataweka milioni 70 kwa ajili ya William Jose, kutakuwa hakuna kilichobakia tena cha kusema”>>>> Imanol

Soma na hizi

Tupia Comments