Michezo

Headlines za Vyombo vya Habari Hispania, hali si shwari Real Madrid…

on

2510F20200000578-0-image-m-38_1422266251437

Nchini Hispania mabingwa wa ulaya Real Madrid huenda wakaingia matatani na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA baada ya shirikisho hilo kuamuru ufanyike uchunguzi kwenye usajili wa wachezaji wenye umri chini ya miaka kumi na nane miaka miwili iliyopita.

Madrid ilisajili wachezaji wawili toka Venezuela ambao ni Mariano Godoy na Fernando Macias mwaka 2012 baada ya kuwapa nafasi ya kufanya majaribio wakati wakiwa ziarani barani Ulaya.

Endapo Madrid watakutwa na hatia huenda wakapewa adhabu sawa na ile waliyopewa fc barcelona ya kutosajili wachezaji katika madirisha mawili mfululizo.

Taarifa hii inakuja baada ya Real Madrid kutangaza kuwasajili wachezaji wawili wenye umri wa miaka 16 ambapo ni Lucas Silva na Martin Odengaard.

Hivi karibuni Real Madrid ilitangaza kumsajili nyota wa Norway Martin Odegaard.

Nyota wa Norway Martin Odegaard.

Endapo Madrid kweli watakumbwa na adhabu ya kuzuiwa kufanya usajili katika madirisha mawili ya usajili itakuwa habari njema kwa viongozi na mashabiki wa klabu kama Manchester United, Chelsea na Manchester City ambazo kwa nyakati tofauti zimejikua zikishindwa na Real katika mbio za kusajili wachezaji nyota.

Zaidi ya hapo pia taarifa itawafurahisha watu wa Manchester United kutokana na jinsi ambavyo kumekuwepo na tetesi zinazoihusisha Real na usajili wa kipa David De Gea.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments