Michezo

Angalia video ya namna Ronaldo alivyompita Messi kwenye rekodi ya magoli ulaya

on

article-2490591-1940E4C000000578-278_636x471Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana alizidi kuisogelea rekodi ya ufungaji bora wa muda wa ligi ya ulaya inayoshikiliwa na Raul Gonzalez Blanco.

Mpaka kufikia jana Raul Gonzalez alikuwa akiongoza listi ya wafungaj bora wa muda wote wa ulaya akiwa na magoli 71, Ronaldo na Messi wakiwa wamefungana wote wakiwa na magoli 68.

Lakini jana Ronaldo akiichezea klabu yake ya Real Madrid jana usiku dhidi ya Ludogorets ya Bulgaria, alifunga goli lake la 69 katika michuano ya ulaya na hivyo kumpita mpinzani wake Lionel Messi mwenye magoli 68.

Mchezo wa jana uliisha kwa ushindi wa 2-1 kwa Real Madrid, Karim Benzema akifunga goli lingine la Madrid.

Angalia magoli hapa chini

Highlights – Ludogorets vs Real Madrid (1-2) 01… by TeQuieroRealMadrid

Tupia Comments