Top Stories

Mikataba Ranchi ya Taifa kilichobainika ndani ya miaka 10

on

Leo October 12,2018 tunayo story kutokea Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ambapo baada ya miaka 10 imebaini kuwa baadhi ya vifungu vya Mikataba havina tija kwa kampuni na wawekezaji.

Kaimu Meneja Mkuu wa NARCO, Prof Philimon Wambura amesema kampuni iliingia mikataba ya uwekezaji kwenye vitalu katika ranchi zake na wafugaji wadogo toka mwaka 2007 kwa nia ya kuwezesha wafugaji wa asili kufuga kibiashara.

“Baada ya miaka 10 kupita, tathmini ya uwekezaji imefanyika na kubaini kuwa baadhi ya vifungu vya mkataba havina tija kwa kampuni na wawekezaji,”amesema.

Kutokana na hatua hiyo, Dk.Wambura amesema NARCO imehuisha mikataba hiyo ya awali ya vitalu na kuja na mikataba mipya.

Amesema kuwa mikataba hiyo imepitia michakato mbalimbali ikiwemo kuwashirikisha wawekezaji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Baba Mzazi wa MO DEWJI “ni kweli Mwanangu ametekwa”

Soma na hizi

Tupia Comments