Michezo

Rekodi za Real Madrid ikitwaa taji lake la 34 la LaLiga

on

Club ya Real Madrid baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Hispania LaLiga 2019/20 kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal, hili ndio linakuwa taji lao la kwanza la LaLiga toka 2017.

Real Madrid hilo ndio linakuwa taji lao la kwanza toka Cristiano Ronaldo aondoke timu hiyo 2018 na kujiunga na Juventus.

Hili ni taji la 34 la LaLiga kwa Real Madrid wakiwazidi wapinzani wao wakuu FC Barcelona kwa tofauti ya mataji 8, Barcelona wakiwa na mataji 26 ya LaLiga.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anakuwa kashinda jumla ya mataji 11 katika jumla ya michezo 209 aliyoiongoza Real Madrid (LaLiga 2, UEFA Champions League 3, UEFA Super Cup 2, Supercopa de Espana 2 na FIFA Club World Cup 2).

Soma na hizi

Tupia Comments