Michezo

Arsenal wakiweka rehani kibarua cha Solskjaer

on


Usiku wa September 30 2019 katika uwanja wa nyumbani wa Manchester United unaofahamika kama Old Trafford, ilichezwa game ya 231 kati ya Man United dhidi ya Arsenal toka wakutane kwa mara ya kwanza.

Man United wakiwa nyumbani wameshindwa kutumia vizuri uwanja wao na kupata point tatu, hiyo inatokana na wao kushindwa kulinda goli lao lililofungwa na McTominay dakika ya 45 ya mchezo lakini Arsenal wakachomoa dakika ya 58 kupitia kwa Pierre Emerick Aubameyang na game kuisha kwa sare ya 1-1.

Sare hiyo ni kama kuweka kibarua cha Solskjaer rehani kufuatia takwimu mbovu za karibuni kiasi cha Man United kuwa nafasi ya 10 kwa kuvuna alama 9 pekee katika michezo saba, ukizingatia mtendaji mkuu wa timu hiyo Ed Woodward kusema kwa wawekezaji kuwa kampa muda Solskjaer wa kuunda timu.

Arsenal sare hiyo wao inawaweka katika nafasi ya nne kwa kuwa na alama 12 baada ya kucheza michezo 7, wakishinda game 3 na kutoka sare game 3 huku wakipoteza game mmoja pekee.

Soma na hizi

Tupia Comments