Kwa Tanzania majengo ya zamani utayakuta katika miji mikongwe kama Bagamoyo, Kilwa, Mikindani, Unguja na Tanga ambapo mengi ya majengo yamekuwa yakitumika kwa ajili ya shughuli za kitalii.
Leo March 16 2017 nimekutana na hii ya migahawa kutoka sehemu mbalimbali duniani ambayo ni mikongwe zaidi na ambayo inaendelea kutoa huduma zake kama kawaida hadi sasa ambapo mgahawa mkongwe zaidi ulijengwa mwaka 803.
1: Stiftskeller St. Peter. – Salzburg, Austria, 803
Huu ndiyo mgahawa mkongwe zaidi duniani ambao umebaki katika miundombinu ile ile ya zamani ambapo ulijengwa mwaka 803 na ulitambuliwa na mwanachuoni Albuin. Baadhi ya sehemu zimefanyiwa marekebisho mara kadhaa lakini kuna baadhi ya sehemu hasa za chakula zimebaki katika sili yake.
2: Bianyifang – Beijing, China, 1416
Kwa sasa Bianyifang haufanyi shughuli zake katika muonekano wa asili lakini bado unatajwa kuwa miongoni mwa migahawa mikongwe zaidi duniani ambayo inaendelea kutoa huduma hadi sasa ambapo ulifunguliwa rasmi mwaka 1416.
3: Zum Franziskaner – Stockholm, Sweden, 1421
Ulianzishwa mwaka 1421 na Watawa wa Kijerumani katika mji wa Old Town Stockholm ambapo Zum Franziskaner umekuwa maarufu kwa watalii wa ndani umefanyiwa maboresho mara kadhaa na muonekano wa sasa ulifanywa mwaka 1906.
4: Honke Owariya – Kyoto, Japan, 1465
Ulianzishwa mwaka 1465 na ndiyo mgahawa mkongwe zaidi Japan na umekuwa ukiwahudumia zaidi watawa na watawala kwa miaka mingi sana.
5: La Tour d’Argent – Paris, Ufaransa, 1582
La Tour d’Argent au “the Silver Tower,” unasemwa ulijengwa na King Henri IV ulianzishwa 1582.
6: Zur Letzten Instanz – Berlin, Ujerumani, 1621
Ulianza kujengwa 1561 lakini haukuendelezwa mpaka 1621 ukiwahudumia karibu kila mtu kutoka Napoleon na Beethoven hadi kwa Angela Merkel na watu wengine wa kimataifa kwa miaka mingi. Jengo la mgahawa huu lilijengwa upya mwaka 1963 baada ya kuharibiwa na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
7: White Horse Tavern – Newport, Rhode Island, 1673
Unatambulika kuwa mgahawa mkongwe zaidi unaofanya kazi nchini Marekani na ni maarufu sana kwa kuuza samaki kutoka Narragansett Bay ambapo ulianzishwa 1673 ambapo mmoja kati ya wamiliki rasmi wa mwanzo alikuwa ni William Mayes Jr.
8: A la Petite Chaise – Paris, Ufaransa, 1680
Ukilindwa na geti lake la asili ambalo ni chuma katika jiji la Paris, A la Petite Chaise umeendelea kutoa huduma zake tangu kuanishwa kwake mwaka 1680 na Georges Rameau aliyekuwa mfanya biashara ya mvinyo. Mgahawa huu umekuwa makutano ya kisiasa, kijamii na sanaa.
9: Botín – Madrid, Uhispania, 1725
Botín ni mgahawa mkongwe duniani, kwa mujibu wa “Guinness Book of Records.” Katikati ya Madrid ulianzishwa 1725 na ulikuwa sehemu ya mikutano.
10: Fraunces Tavern – New York, N.Y. 1762
Kwa upande wa historia ya Marekani Fraunces Tavern ulikuwa kitovu kikubwa cha kuibadilisha Marekani ambapo mara ya kwanza uliitwa Queen’s Head mwaka 1762 na Samuel Fraunces ambaye aliununua kutoka kwa shemeji wa Meya wa New York City Stephanus van Cortlandt.
VIDEO: Uliikosa hii ya mpango mwingine wa RC Makonda kwa waathirika wa Dawa za Kulevya? Bonyeza play hapa chini kutazama.