Michezo

Ninayo ya Arsenal VS AS Monaco hapa mtu wangu..

on

Ars II

Olvier Giroud na Aaron Ramsey walikuwa mashujaa siku ya jana kwa kuisaidia timu yao ya Arsenal kumaliza safari yao kwenye ligi wakiwa na ushindi mezani.

Arsenal walikuwa wakipambana na timu ya AS Monaco na Arsenal wakaibuka na ushidni wa mabao 2-0.

Ushindi huo hauna matunda yoyote kwa Arsenal, wametolewa kwenye Ligi ya Mabigwa Ulaya ambapo ligi hiyo imefikia hatua ya robo.

Nyumbani kwao Arsenal walifungwa 3-1 wakiwa Uwanja wa Emirates, hivyo ushindi wa jana haukutosha kuwafanya waendelee na safari ya ligi hiyo.

Ars

Wachambuzi wa soka wanasema japo Monaco wamesogea hatua moja kubwa mbele kwenye ligi hiyo, mchezo wao haukuwa kwenye kiwango kizuri japo walikinga kifua kwa nguvu zote kuhakikisha Arsenal haiwafungi zaidi ya goli 2.

Ars III

Ars IV

Ars V

Kwenye Facebook, Instagram na Twitter natumia jina la millard ayo mtu wangu, jiunge na mimi niwe nakusogezea kila taarifa inayonifikia, kujiunga na mimi bonyeza >>>twitter Insta Facebook 

Tupia Comments