Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameagiza Halmashauri nchini kutoa mikopo kwa Vijana, wanawake na watu walemavu hadharani na kwa uwazi mkubwa ili kuondoa malalamiko ya watu kudai mikopo hiyo haitolewi na kusaidia kupunguza changamoto ya ajira Dar es Salaam.
RC Makalla ameyasema hayo leo, wakati wa kikao chake na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Mameya na wadau wa mikopo hiyo ya Halmashauri huku akihimiza fedha hizo kuwafikia wanufaika waliokusudiwa na Serikali.
Aidha RC Makalla amezitaka halmashauri kuandaa maonesho ya bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vinavyokopeshwa na halmashauri, ili kuzitangaza zaidi.
Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo amebainisha kuwa bado hawajapata mafunzo ya matumizi ya fedha hizo pamoja na kukosa masoko ya bidhaa zinazozalishwa na vikundi vinavyokopeshwa fedha hizo.