Habari za Mastaa

Majibu ya kuchelewa kwa video ya Roho yangu ya Rich Mavoko haya hapa.

By

on

mavokoMpaka sasa tayari video ya Rich Mavoco ya Roho yangu haijatoka rasmi ingawa ilishatoka taarifa ya kukamilika kwa hiyo video,millardayo.com imeongea na Rich Mavoco kuhusu hii video kwa kuzingatia kwa sasa ameshafanya show kadhaa zilizohusisha uzinduzi wa video hiyo.

Rich Mavoco analo lakujibu kuhusu swali hili  alianza kwa kuelezea juu ya Gharama za video hiyo>>’Kuhusu gharama mpaka sasa hatujapata gharama kamili maana video mpaka sasa kuna vitu hatujamalizia nategemea siku chache zijazo ndiyo tuizindue maana hii video tumefanya mara mbili’

‘Video tuliletewa usiku kuna baadhi ya vitu kwa maoni ya watu walisema turekebishe,sisi tunaishi na watu pia na sisi tupo ndani ya mchezo so kocha aliye nje ndiye anayeona mpira vizuri kuliko mchezaji wa ndani so walivyosema watu wetu wa karibu ikabidi tumwambie director arekebishe na Director wa video hii ni Meja.’

Mavoko pia katoa Exclusive kuhusu Collabo yake na vijana toka ardhi ya 256 hawa ni Radio&Weasel  ambapo taarifa ya Collabo hii amesema bado haijawa rasmi lakini anategemea kufanya nao kazi muda si mrefu.

 

Tupia Comments