Habari za Mastaa

Rick Ross ajibu tuhuma za ubakaji dhidi yake…

on

Siku chache zilizopita Rick Ross aliweka headlines baada ya mwanamke ambaye jina lake halijatajwa kumshtaki rapper huyo na rafiki yake kwa ubakaji… mwanamke huyo alidai kuwa alifuatwa na rapper huyo pamoja na marafiki zake kwenda kwenye party huko Los Angeles na badaae wakamchanganyia vitu kwenye kinywaji chake vilivyofanya apoteze fahamu na kubakwa.

rosey2

Rapper Rick Ross.

Japo yeye sio alietajwa kama mbakaji bali kama mtu aliemtengenezea rafiki yake mazingira ya yeye kufanya kitendo hicho, Rick Ross amechukuwa time na kujibu tuhuma hizo dhidi yake kupitia mtandao wa TMZ Marekani na kusema…

>>> “Nimefahamishwa juu ya tuhuma nzito dhidi yangu na kijana ambaye huwa namtumia kwenye kazi zangu nyingi, na wakati mimi sio ambaye nahusika moja kwa moja lakini kama mwanaume na baba tuhuma hizo nazichukulia kwa uzito mkubwa sana. Siamini usalama wa mwanamke yoyote unastahili kuchukuliwa poa na huwa naamini kuwa mwanake hatakiwi kulazimishwa kufanya kitu chochote ambacho hapendi au hataki licha ya mazingira yaliopo. Mimi binafsi sina taarifa yoyote wala maelezo halisi ya nini kilitokea siku ile na natumaini issue hii haitachukuliwa poa bali isikilizwe kwa umakini na uzito mkubwa!” <<< Rick Ross.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments