fB insta twitter

Alichoandika Maximilian baada ya kumsikia Young Dee kwenye Radio

on

Aliyekuwa msimamizi wa Rapper Young Dee, Maximilian Rioba ametumia account yake ya Twitter kuandika ya moyoni mara tu baada ya Young Dee kudai hakuchoka kufanya kazi naye bali yeye ndiye alishindwa kufanya kazi na yeye.

Baada ya kauli hiyo ya Young Dee, Max aliandika kupitia account yake kuwa kulikuwa na haja ya media kutaka kujua naye kwa upande wake ili watu waelewe kwa kuwa taarifa aliyoitoa Young Dee haipo kama ilivyosemwa akikumbusha watu kuwa hata yeye alishawahi kutukanwa hadharani.

“Kuna haja ya Media kujaribu kubalance taarifa ili wasikilizaji waelewe mambo Kama yalivyo sio kama yalivyosemwa! niliwahi kutukanwa sana, nidhamu ni nguzo ya mafanikio kila mahali ikivurugwa hiyo hata ungeishi mbinguni utaporomoka tu’

“Tutarejea, hii movie nadhani tulishawahi kuiona, kuna magari yalinunuliwa sijui yalienda wapi? so sad for the kids in the game” – Maximilian Rioba.

EXCLUSIVE: Flora amewajibu wanaosema kamzidi umri Mume wake mpya, ni kweli alimualika Mume wa zamani kwenye harusi yake? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments