Bunge la Seneti la nchini Kenya limepitisha kura ya kumuondoa madarakani aliyekuwa Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua.
Mwanasiasa huyo, alikuwa anakabiliwa na mashitaka 11, na iliwahitaji maseneta hao 67, kupitisha walau shitaka moja tu; ili Gachagua ang’oke madarakani.
Oktoba 17, jumla ya Maseneta 49 walipiga kura ya kumuondoa madarakani aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba ya nchi hiyo.
Mwanasiasa huyo alikuwa akikabiliwa na mashitaka 11, huku akishindwa kutokea na kujitetea mbele ya Bunge la Seneti Oktoba 17, baada ya wakili wake kusema kuwa yuko hospitali akipokea matibabu.
Kulingana na katiba ya Kenya, Naibu Rais anafikia ukomo wa nafasi hiyo baada ya kuondolewa na Bunge la Taifa na Bunge la Seneti la nchi hiyo.