Rigobert Song sio kocha wa timu ya taifa ya Cameroon “Indomitable Lions” tena ametangaza rais wa shirikisho la soka la Cameroon (Fécafoot) Samuel Eto’o, siku ya Jumatano jioni katika mahojiano na France 24.
“Hatujafikia malengo yetu, na kamati yetu ya utendaji na mimi hatuoni tukiongeza mkataba,” ameeleza mkuu wa Fécafoot.
Cameroon ilitolewa katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Afrika mwezi Januari na Nigeria (2-0).
Aliyeteuliwa mwanzoni mwa mwaka2022, “Rigo” alianza majukumu yake kwa kufuzu kwa miujiza kwa Kombe la Dunia dhidi ya Algeria, kwa bao katika sekunde za mwisho baada ya bao la Algeria (0-1/2-1 ap).
Huko Qatar, Cameroon ilitolewa katika raundi ya kwanza lakini ikatoka na ushindi wa hali ya juu dhidi ya Brazil (1-0).
Katika mechi 23 , bingwa wa Afrika mara mbili (2000 na 2002) ameshinda mechi 6 tu, huku ikihindwa mara 9 na kutoka sare 8.
Rigobert Song “alileta mengi kwa timu hii”, ameongeza Eto’o, akitoa “sifa nzuri kwa Rigobert Song ambaye alikuwa nahodha (wake) katika timu ya taifa”.