Habari za Mastaa

Album mpya ya Rihanna ipo njiani, na hili ndio dili nono la kudhamini Album hiyo!

on

Rihanna kwenye healines mtu wangu, baada ya kutudokeza cover mpya ya Album yake mpya ‘Anti’ msanii huyo pamoja na management yake imeamua kuingi mkataba na kampuni kubwa ya simu duniani, Samsung kwa ajili ya kudhamini na kupromote ujio wa Album hiyo pamoja na Tour yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa New York Post, mkataba wa Rihanna na Samsung utakuwa wa miezi saba baada ya msanii huyo kuamua kufanya mabadiliko kadhaa kwenye Album yake mpya ya ‘Anti’.

SAMRIRI3

Jay Z amabaye ndiye Mkurugenzi wa Roc Nation label aliyopo Rihanna  na Jay Brown ambaye ndiye Manager wa msanii huyo walisaidiana kukamilisha dili hiyo lenye thamani ya dola Milion 25 sawa na Tzs. Bilion 55 kwa niaba ya Rihanna.

Kampuni hiyo ina mipango ya kushirikiana na lebo ya Rihanna, kwa ajili ya kufanikisha mpango huu ambapo pia Roc Nation lebo ya Rihanna inafahamika kuwa na historia nzuri ya mahusiano na kampuni hiyo ya simu ambayo mwaka 2013 kampuni hiyo kutoka South Korea ilinunua zaidi ya copy milioni moja ya Album ya Jay Z, Magna Carta.

SAMRIRI2

Kwa sasa lebo ya Roc Nation na Rihanna mwenyewe bado wanajadiliana tarehe nzuri ya kuileta sokoni Album mpya ya msanii huyo.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments