Michezo

Rio Ferdinand awatoa Messi na Ronaldo ampa Mbappe

on

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe, raia wa Ufaransa atachukua ufalme wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kutokana na kuonyesha kiwango kizuri tangu alipotua katika klabu hiyo akitokea Monaco miaka mitatu iliyopita.

Ferdinand ametoa kauli hiyo baada ya nyota huyo kufunga ‘hat-trick’ katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Barcelona uliopigwa Jumatano iliyopita ambapo PSG, iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Sio Ferdinand tu aliyemmwagia sifa Mfaransa huyo bali pia kiungo wa zamani wa Manchester United, Owen Haegreaves amemlinganisha Mbape na mbrazil Ronaldo De Lima kwa namna anavyojua kucheka na nyavu.

MTANZANIA AUNDA MAGARI, CROWN ATHLETE IPO, ANAPIGA HELA “WAZUNGU WANANUNUA”

Soma na hizi

Tupia Comments