Michezo

Rio Ferdinand kuhusu Mino Raiola kutaka kumuondoa Pogba Man United

on

Wachezaji wa zamani wa Man United Paul Scholes na Rio Ferdinand wameoneshwa kukasirishwa na kitendo cha wakala wa Paul Pogba anayejulikana kwa jina la Mino Raiola kueleza kuwa Pogba hana furaha Man United.

Ferdinand ameeleza kusikitishwa na mtendaji mkuu Man United Ed Woodward na kocha Ole Gunnar Solskjaer kuwa kimya chao kimemfanya Mino Raiola kuipanda Man United kichwani.

“Inakuwaje una mruhusu wakala wa mchezaji kuongea maneno kama haya? hii sio mara ya kwanza anafanya hivyo, inatakiwa unamfunga mdogo pale tu alipofanya kwa mara ya kwanza”>>> Rio Ferdinand

“Man United haitakiwi kumsubiri mchezaji ndio aongee, hawatoimarika mchezaji ndio anamuendesha wakala, huwezi kuruhusu ili litokeaa”>>> Ferdinand VIA BT Sports

Soma na hizi

Tupia Comments