Michezo

Ya moyoni mwa Rio Ferdinand kuhusu kuondoka Man Utd

on

article-2626517-1DCBF91700000578-78_964x386Jana usiku maisha ya kisoka ya beki wa kimataifa wa England Rio Ferdinand ndani ya klabu ya Manchester United yalifikia mwisho baada ya kutangaza kwamba ameamua kuachana na klabu hiyo.

Rio Ferdinand ambaye alijiunga na Manchester United mnamo mwaka 2002 kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya uhamisho paundi millioni 29.5 ameshaitumikia United kwenye michezo 454 na amemaliza mkataba wake na klabu hiyo na pande zote mbili zikaamua kutoongeza mkataba mpya.

Muda mfupi baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao kuhusu kuondoka United, Ferdinand alitumia mtandao wake binafsi kutoa rasmi taarifa ya kuondoka Old Trafford.

>>> ‘Nimekaa nikiwaza kwa miezi kadhaa sasa juu ya siku zangu za mbeleni na baada ya miaka 12 mizuri kabisa ya kuchezea timu ambayo kwangu ndio nzuri kuliko zote duniani, nadhani ni muda wa kuendelea na maisha mengine’

>>> ‘Nilijiunga Manchester United nikiwa na tegemeo la kushinda makombe na sikuwahi kuwaza kama tutafanikiwa vile ndani ya muda wangu hapa United, kucheza na wachezaji wazuri ambao pia ni marafiki, kushinda kombe la Premier league kwa mara ya kwanza pia ule usiku mzuri Moscow…. hivi ni vitu nitakumbuka maishani mwangu’

>>> ‘Changamoto hazinuruhusu mimi kuaga nilivyotaka lakini napenda kuchukua nafasi hii kushukuru wachezaji wenzangu, wafanyakazi, club kwa ujumla na mashabiki wangu kwa miaka 12 ambayo sitaweza kuisahau, kushinda makombe ambayo niliyaota nikiwa mdogo’

>>> ‘Najisikia vizuri mwenye afya na nipo tayari kwa chochote ambacho kitakuja kwangu siku za mbeleni’

Vitu kama hivi ni halali yako visikupite… niko tayari kukutumia kwenye twitter instagram na facebook kila zinaponifikia iwe usiku au mchana, jiunge na mimi kwa kubonyeza HAPA na >> INSTA na FB

 

 

Tupia Comments