Mpira wa miguu ni mchezo uliyoteka hisia za watu wengi na ndio mchezo unaohusisha wachezaji 11 na shabiki anatajwa kuwa mchezaji wa 12 kwa kazi yake ya kushangilia tu, inaaminika kuongeza hamasa kwa wachezaji wa timu anayoishangilia ili waweze kucheza vizuri.
Unamkumbuka Steven wa Yanga yule jamaa aliyelia wakati Yanga ilipofungwa na Simba kwa idadi kubwa ya magoli, basi sio yeye tu ndio maarufu katika suala la kushangilia kuna mzee anaitwa Clovis Acosta Fernandes ambaye alipata umaarufu na kuingia katika headlines kwa kulia baada ya timu yake ya taifa ya Brazil kufungwa goli 7-1 na Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
Kwa bahati mbaya ni kuwa Clovis Acosta Fernandes amefariki akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kansa kwa miaka 9. Hili ni pigo kwa Brazil kwani wamempoteza moja kati ya watu wao mahiri katika suala la ushangiliaji.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos