Ajali

Salamu kutoka kwa Rais Magufuli kwa waathirika wa ajali ya December 18 Iringa..

on

December 18 2015 nilikusogezea ripoti kutoka Iringa Tanzania, ilihusu ajali ya basi la abiria la Kampuni ya New Force Ltd ambalo lililongana na lori la mbao lilibeba mbao kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam… watu 12  walifariki na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa wote waliofariki kwenye ajali hiyo.

Kwenye barua hiyo toka Ikulu, hii ni nukuu ya alichokisema Rais Magufuli >> ‘Nimesikitishwa sana kutokea ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao na ninawaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao‘- Rais John P. Magufuli.

Barua yote kutoka Ikulu ii hapa

RAIS JPM

Wapumzike kwa amani marehemu wote, na wale majeruhi MUNGU awatie nafuu wapone haraka.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments