Ad
Ad

Habari za Mastaa

Taarifa za awali kuhusu kifo cha Director Adam Kuambiana.

on

DSC02051Hizi ni taarifa zingine za ghafla ambazo Tanzania tumezipokea kwa mshtuko na masikitiko ni kifo cha miongoni mwa-madirector wa Tanzania ambao ni waigizaji pia,huyu ni Adam Kuambiana ambaye taarifa za kifo chake zimeanza kusambaa mchana wa Mei 17.

DSC00263Marehemu Adam Kuambiana akiwa location enzi za uhai wake.

Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema>>’Mwenzetu Adam Philipo Kuambiana amefariki akiwa Location ana shoot,mimi nimepigiwa simu saa 3 asubuhi kuwa hospitali pale Mwenge niende nikahakikishe kuwa ni kweli Adam amefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam Kuambiana amefariki’

‘Sasa hivi tumetoka Muhumbili kwenda kumsitiri mwenzetu,taarifa inasema wakati yupo location alikua analalamika tumbo linamuuma linamuuma kumfikisha hospitali ndipo umauti ukamfika’.

Kwa mujibu wa Steve Nyerere amesema kuwa marehemu Adam kuambiana alikua ana shoot filamu yake mpya ambayo ndani yake amewashirikisha wasanii kadhaa wa Bongo fleva akiwemo Q Chillah,taratibu za mazishi na msiba kwa ujumla endelea kufatilia millardayo.com nitakufahamisha kila kinachoendelea.

Bonyeza play kumsikiliza Steve Nyerere akielezea msiba huu.

Tupia Comments