Ajali

Sentensi 10 za mke wa Marehemu kuhusu ajali, picha za Marehemu na kifo cha Mchungaji Mtikila..

on

October 22 2015 ni wiki ya tatu zimepita tangu aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila afariki kwa ajali ya gari ndogo eneo la Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani.

Rais JK akimpa pole Mama Georgia Mtikila siku mwili wa Mrehemu Mtikila ulipoagwa Viwanja vya Karimjee Dar.

Rais JK akimpa pole Mama Georgia Mtikila siku mwili wa Marehemu Mtikila ulipoagwa Viwanja vya Karimjee Dar.

Mama Georgia Mtikila ni mke wa Marehemu Mchungaji Mtikila… leo kwa mara ya kwanza amekutana na Waandishi wa Habari Dar es Salaam na kuzungumzia kuhusu kifo cha mumewe >>>> “Kuna habari ilitoka kwamba familia imesema ajali ya Mchungaji Mtikila ni ya kawaida.. naipinga, aliyetoa taarifa hiyo hakuwa mwanafamilia na sio Mwanachama wa DP… Hakuna Mwanafamilia aliyekuwa tayari kutoa taarifa yoyote kwa niaba ya Chama wala Familia.”

IMG-20151004-WA0006

Naomba tusaidiwe ili haki ya Marehemu ionekane ikitendeka, haya maombi tunaomba yafike…. Tunaomba Rais aingilie kati kwa kuunda Tume huru isiyohusisha Polisi ili kuchunguza kifo cha Mchungaji Mtikila” >>> Mama Georgia Mtikila.

MTIKILA

Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila.

Tunaiomba TCRA itusaidie kumpata mtu aliyeweka picha ya Marehemu Mtikila alfajiri siku ya ajali, kwa sababu mpaka sasahivi simu ya Mchungaji hatujui iliko…” >>> Mama Georgia Mtikila.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments