Rais Cyril Ramaphosa wa South Africa amesema leo kuwa Taasisi za usalama Nchini humo zimewatambua watu kadhaa wanaoshukiwa kuchochea vurugu wiki hii.
Ramaphosa ameyasema hayo alipotembelea Manispaa ya Ethekwini ambayo inajumuisha mji wa bandari wa Durban, moja ya maeneo yaliyoathirika pakubwa katika wiki nzima ya uporaji ambao uliharibu mamia ya maduka na kuwauwa zaidi ya Watu 100.
Rais huyu amesema pia Wanajeshi 25,000 watapelekwa katika maeneo yenye vurugu hivi karibuni na hiyo itakua imeongeza idadi ya Wanajeshi mitaani kutoka 10,000 ambayo tayari wameshaingizwa mitaani.
Ramaphosa amesema waliochochea vurugu hizo wanasakwa na pia utulivu umeanza kurejea kwa sehemu katika mji mkuu wa kibiashara Johannesburg japo maduka mengi bado yamefungwa na operesheni katika bandari za Durban na Richards Bay zinaimarika.