Top Stories

Ripoti kutokea Mwanza aliefyatua risasi kumuenzi Marehemu

on

Mtu mmoja aitwae Silas Charles (45) ambae ni Mfanyabiashara wa Samaki Jijini Mwanza amefariki kwa kupigwa risasi msibani jana Jijini Mwanza katika kisa ambacho sio cha kawaida baada ya kumaliza kumzika Jamaa yake.

Mauaji hayo yalitokea wakati Waombolezaji wakiwa maeneo ya makaburi ya Kangae ambapo risasi iliyomuua Silas ilifyatuliwa na Muombolezaji mwenzake aitwae Jacobo Amoro (60) ambae alisema anafyatua risasi angani akidai ni ishara ya kumpa heshima za mwisho Marehemu.

Wakati Jacobo akifyatua risasi hizo kwa bahati mbaya moja ilimlenga Silas na kufariki palepale eneo la tukio na kusababisha Waombolezaji wengine kukasirika na kuanza kumpiga Jacobo na kumsababishia majeraha ambayo anatibiwa Hospitali Jijini Mwanza chini ya ulinzi wa Polisi.

“Mtuhumiwa Jacobo ni Mkazi wa Dodoma na alikua amekuja hapa Mwnaza kuhudhuria mazishi ya Jamaa yao aitwae William Okoo, alikua akimiliki bastola hiyo kihalali lakini amekiuka masharti ya leseni yake na tunamshikilia chini ya ulinzi Hospitali” ——— RPC Mwanza Ramadhan Ng’azi.

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA PAPOHAPO NA POLISI ”WALITAKA KUTEKA MAGARI BARABARANI”

KUJIUZULU KWA MO DEWJI, EDO KUMWEMBE AMTETEA, HAJI MANARA NA MPOKI WATIA NENO

 

 

Tupia Comments