Manchester City wanaweza kuwa na faida zaidi ya wapinzani wao ikiwa wanataka kumsajili fowadi wa Napoli Khvicha Kvaratskhelia msimu huu wa joto, kulingana na wakala wake.
Akiongea na kituo cha Georgia 1TV Sport, mwakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 Mamuka Jugeli alisema: “Napoli waliongeza mkataba wa [Victor] Osimhen, lakini Khvicha hangekubali uhamisho wa kwenda Saudi hata kama angempa euro bilioni.
“Kwa mfano, pengine angekubali kuchezea Real Madrid, Bayern Munich, Barcelona au Manchester City.
Khvicha ana matamanio na malengo tofauti: anataka kufanikiwa, na tayari anafanikisha.”