Michezo

Mtoto wa mchezaji bora wa dunia kutokea Brazil amejiunga na klabu hii ya Ureno….

on

Mtoto wa mchezaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Rivaldinho Rivaldo ambaye anafuata nyayo za baba yake Rivaldo katika soka, amesajiliwa na klabu ya Boavista ya Ureno akitokea klabu ya Mogi Mirim ya kwao Brazil. Hivyo hiyo inakuwa mwanzo wa safari yake ya kusaka mafanikio kama aliyoyapata baba yake Ulaya.

ng887322E8-A487-4317-B9AD-945B6421D929

Rivaldinho ambaye ana umri wa miaka 20 amejiunga na klabu ya Boavista kwa mkataba wa miaka mitatu na kuhama katika klabu ambayo baba yake mzazi ni Rais, hiyo itamfanya kukua na kukomaa kisoka kwani ataanza kuishi mbali na uangalizi wa baba yake.

ng4618719

Mchezaji huyo ambaye amepata umaarufu kutokana na ukubwa wa jina la baba yake, ni kawaida kuingia katika headlines kila mara anapofunga goli, ameichezea klabu ya Mogi Mirim jumla ya mechi 44 na kufunga goli 10. Rivaldinho ili aweze kufikia rekodi za baba yake inabidi ajitume kwani hadi sasa hajawahi cheza katika timu ya taifa ya Brazil hata ya vijana.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikiaza siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments