Habari za Mastaa

R. Kelly anaisogeza kwetu official video ya mdundo wake mpya; ‘Backyard Party’ – (Video).

on

Mara ya mwisho tumemsikia R. Kelly ilikuwa miezi michache iliyopita ambapo msanii huyo wa R&B aliachia single yake ya ‘Backyard Party’ wimbo uliofanya vizuri kwenye chati mbalimbali za muziki Marekani… Kama wewe ni shabiki wa R. Kelly basi ikufikie kuwa official video ya ‘Backyard Party’ imetoka na ipo hewani tayari.

Kellz

R. Kelly kwa sasa yupo anamalizia Album yake mpya The Buffet, album inayotegemea kuwa sokoni tarehe 20 November 2015 na kwa mujibu wa Kellz mwenyewe msanii huyo amesharekodi nyimbo 462 kwa ajili ya album yake mpya na anachokifanya sasa hivi ni kuchagua ni nyimbo gani zitakazoibeba albuma yake mpya…

>>> “Siku zote nimekuwa nikipenda kufanya miziki ya aina tofauti na pia kuongelea vitu tofauti, na album hii imenipa chance ya kufanya hivyo vyote… mashabiki wategemee vitu vizuri kutoka kwangu this time.” <<< R. Kelly aliuambia mtandao wa EW.

Nimekusogezea official video ya R. Kelly hapa chini mtu wangu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments