Habari za Mastaa

R Kelly akwepa maswali, ni kuhusu mtoto wake kubadilisha jinsia.

on

jaya-kelly-21

Mwanamziki wa Marekani Robert Kelly maarufu kama R.kelly amekataa kujibu maswali yanayomhusu mtoto wake wa kike Jaya kubadilisha jinsia.kuwa wa kiume.

rkelly-jay-kelly-550

R Kelly amekuwa akikwepa kujibu maswali hayo juu ya hatua ya mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 aliyotangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa amebadilisha jinsia yake na kuwa wa kiume akijiita Jay Kelly.

jaya

Mwanamuziki huyo maarufu kutoka nchini Marekani amesema kuwa hatopenda kulizungumzia suala hilo la mtoto wake kujibadili jinsia na kuongeza kuwa hata kama kuna ukweli wowote hatovipa vyombo vya habari uhuru wa kuzungumzia.

 

R Kelly ameongeza kuwa ni vyema watu wakaamini wanachokiona kwa macho kuliko wanachosikia kwani hata yeye amesikia juu ya suala hilo lakini si kweli.

R Kelly amebarikiwa kuwa na watoto wengine wawili Joann Kelly na Junior Robert Kelly aliozaa na mke wake wa zamani Andrea Kelly.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB

Tupia Comments