Hali ya hewa haikuwa sawa Hispania baada ya Real Madrid kumaliza msimu bila ushindi wa Taji lolote, maamuzi magumu yakafanya kwa kumsimamisha aliyekuwa Kocha wa Klabu hiyo, Carlo Ancelotti.
Klabu ya Real Madrid imemthibitisha Mhispania Rafael Benitez kama kocha wake mpya zikiwa zimepita siku mbili tangu kocha huyo alipoachana na klabu yake ya zamani ya Napoli.
Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid, ana historia ndefu ndani ya klabu hiyo… aliwahi kuichezea akiwa kwenye kikosi cha vijana kabla ya kuwa kocha wa timu za vijana na baadae kikosi cha kwanza akiwa chini ya Vicente Del Bosque.
Madrid imethibitisha kuwa Benitez ametia saini mkataba wa miaka mitatu na ataanza kazi yake mara tu baada ya mapumziko baada ya msimu wa ligi za soka barani Ulaya kumalizika.
Kwa muda mrefu tetesi zilimhusisha Benitez na kujiunga na Real ambapo siku hadi siku tetesi hizo zilizidi kupata nguvu mpaka hii leo ambapo imethibitika rasmi kuwa Benitez ndio kocha mpya wa Real Madrid.
Kabla ya Real Madrid, Benitez aliwahi kuwa kocha wa Valencia, Liverpool, Inter Milan, Chelsea na Napoli ambako akiwa na Valencia, Chelsea, Liverpool na Inter Milan amewahi kutwaa mataji makubwa ikiwemo ligi ya Hispania, Ligi ya Mabingwa, ligi ya UEFA, Europa na kombe la dunia kwa klabu.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.