Michezo

Headlines zimeanza kupambwa, mpaka mwisho wa wiki huyu kipa atakua kasaini Madrid?

on

balon-oro-real-madrid

Moja kati ya Story ambazo zimeteka hisia za mashabiki wengi wa soka bila kusahau vyombo vya habari za michezo bila shaka ni story ya usajili wa kipa Mhispania David De Gea ambaye ulimwengu mzima unafahamu kinachoendelea kati yake na klabu mbili za Real Madrid na Manchester United.

Jarida moja la kila siku Hispania limeripoti kuwa kipa huyu atakuwa mchezaji wa Real Madrid mpaka ifikapo jumamosi ya wiki hii wakati ambapo Ligi Kuu ya England itakapokuwa ikianza rasmi msimu wake wa 2015/2016.

Taarifa hii inazidi kupata nguvu kutokana na tetesi ambazo zilizuka hapo jana ambapo kocha wa United, Louis Van Gaal aliripotiwa kusema kuwa angependa kuona De Gea akiuzwa kutokana na hali inayoendelea kuleta sintofahamu ndani ya timu.

Madrid watamsajili De Gea mpaka kufikia jumamosi ya wiki hii .

Madrid watamsajili De Gea mpaka kufikia jumamosi ya wiki hii.

Real Madrid imepanga kumfanya De Gea kuwa kipa wake namba moja baada ya kuondoka kwa Iker Casillas ambaye ameitumikia Madrid kwa muda wa miaka 25 karibu miaka 18 kati ya hiyo akiwa kipa namba moja.

Endapo United itakubali kumuuza De Gea katika wakati huu huenda wakajikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kutokuwa na mtu ambaye timu hii imemuandaa kuwa mrithi wa De Gea huku wakiwa hawajaanza mazungumzo na kipa yoyote yule.

Kulikuwa na stori kwamba United imekuwa ikiigomea Madrid kuhusu De Gea huku wakisema wanahitaji kulipwa pound milioni 40 kwa ajili ya kipa huyo na Madrid wakiwa tayari kulipa pound milioni 25 pekee.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments