Michezo

Umeona mastaa wa Club ya REAL MADRID wanavyojiachia? Cheki PICHAZ..

on

9

Mchezo wa soka kwa hatua ilioufikia kwa sasa ni biashara kubwa sana ambayo inategemea uwekezaji mkubwa sana ili iweze kuendelea.

Pamoja na ukweli kuwa huu ni mchezo mwepesi ambao huhusisha wachezaji 22 wanaopambana uwanjani, ushindi husakwa kwa njia za kisasa kwa miaka ya hivi karibuni njia ambazo zinahusisha teknolojia ya hali ya juu ambayo kila siku inaboreshwa.

Klabu ya Real Madrid ni mfano wa hatua hii ambayo imefikiwa kwenye mchezo wa soka, makao makuu ya Real Madrid yanaakisi aina ya maendeleo ambayo klabu ya ukubwa wake inapaswa kuwa nayo.

Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wanawaonyesha waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo .

Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wanawaonyesha waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo.

Klabu hii inamiliki jingo kubwa la makao makuu ambalo ndani yake kuna kila kitu kuanzia viwanja vya kisasa mpaka vyumba vya kupumzikia wachezaji hasa wakati wakiwa kwenye maandalizi ya kuelekea mechi kubwa.

Ukiachilia mbali viwanja na vyumba bora vinavyowahakikishia wachezaji mapumziko mazuri , eneo hilo lina vyumba vya kupumzikia ambavyo vina mashine za michezo ya kompyuta maarufu kama Video Games au Playstation pamoja na michezo mingine kama basketball na volleyball.

Mchezaji wa Real Madrid Assier Illarramendi akiwa kwenye chumba cha michezo cha makao makuu ya klabu hiyo .

Mchezaji wa Real Madrid, Assier Illarramendi akiwa kwenye chumba cha michezo cha makao makuu ya klabu hiyo.

Huu ni mlano wa chumba cha Gareth Bale.

Huu ni mlango wa chumba cha Gareth Bale.

Milango ya vyumba hivi hufunguliwa kwa mfumo wa kisasa wa usalama ambao huhusisha alama za vidole .

Milango ya vyumba hivi hufunguliwa kwa mfumo wa kisasa wa usalama ambao huhusisha alama za vidole .

Hivi ndivyo ilivyo mandhari ya vyumba vya kulala vya wachezaji wa Real Madrid.

Hivi ndivyo ilivyo mandhari ya vyumba vya kulala vya wachezaji wa Real Madrid.

Ndani ya vyumba vya kulala wachezaji kuna televisheni maalum ambazo zinaonyesha taarifa mbalimbali kuhusu wachezaji.

Ndani ya vyumba vya kulala wachezaji kuna televisheni maalum ambazo zinaonesha taarifa mbalimbali kuhusu wachezaji.

Makao makuu ya klabu hiyo yamenakshiwa na picha za magwiji wa zamani pamoja na mataji ambayo Madrid imewahi kutwaa .

Makao makuu ya klabu hiyo yamenakshiwa na picha za magwiji wa zamani pamoja na mataji ambayo Madrid imewahi kutwaa.

Huu ni mgahawa ambao wachezaji hupata chakula wakati wakiwa kwenye maandalizi ya mechi .

Huu ni mgahawa ambao wachezaji hupata chakula wakati wakiwa kwenye maandalizi ya mechi.

Soma na hizi

Tupia Comments