AyoTV

VIDEO: Rais Magufuli alivyotangaza kutengua ukuu wa mkoa wa Anne Kilango Shinyanga

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli April 11 2016 ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela na katibu tawala wa mkoa huo Abdul Rashid Dachi baada ya mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna Watumishi hewa.

Rais Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana Aprili, 10 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.

>>>’Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?’-Rais Magufuli

MTAZAME HAPA CHINI RAIS MAGUFULI ALIVYOTANGAZA KUTENGUA UKUU WA MKOA WA  ANNE KILANGO MALECELA

ULIKOSA MKWARA WA WAZIRI SIMBACHAWENE KWA WAKUU WAPYA WA  MIKOA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments