Habari za Mastaa

Mke wa Roma Mkatoliki hana noma na umaarufu wa mume ila kuna hii ilimkasirisha

on

Wanasema ni ngumu kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu maarufu na kama utakubali kuwa kwenye uhusiano huo basi inabidi uwe muelewa na mvumilivu maana utayoyasikia ni mengi.

Mama Ivan ambaye ni mke wa msanii wa hiphop Tanzania Roma Mkatoliki anasema amezoea kuona headlines za mume wake magazetini lakini kuna moja ilimuumiza na hajaisahau mpaka leo.

>> ‘Mimi sipendi skendo kuhusiana na mume wangu kikubwa na kusema ukweli ilitokea moja kwenye Magazeti kwamba Roma kuwa ana mtoto amezaa na Lotus iliniuma sana moyoni lakini mwisho wa siku nikabaini kwamba si kweli bali zilikuwa ni skendo

Sikuipenda hiyo sana kabisa, mengine yote huwa nayaona kawaida ila hiyo iliniumiza               na nilimuuliza akaniambia sio kweli bahati nzuri alinieleza na nikajua sio kweli‘ – Mama Ivan

ULIIKOSA HII YA HARUSI YA ROMA MKATOLIKI ILIVYOKWENDA KUANZIA KANISANI MPAKA UKUMBINI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments