Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Habari za Mastaa

VIDEO: Maneno ya Rammy Galis juu ya kuvunjika uhusiano wake na Agness Masogange

on

Muigizaji wa kiume anaefanya vizuri katika tasnia  ya Bongo Movie Tanzania, Rammy Galis leo November 18 2016 anatusogezea story kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na mrembo Agnes Masogange  ambapo inadaiwa mapenzi yao yamevunjika, na zile ishu za kutopostiana katika mitandao ya kijamii hazipo tena. 

Rammy ameongea na AyoTV na millardayo.com ambapo ameyaungumza haya…….>>>“Unajua mahusiano ni mahusiano tu, hakuna lenye mwanzo linakosa mwisho hakika yale yalikua ni mahusiano na hakika yamefika mwisho, kwa hiyo sidhani kama nina jambo la zaidi la kulizungumzia zaidi ya hilo siwezi nikaweka tofauti zetu hadharani, ilikuwa ni mahusiano na yameishia.” – Rammy Galis

VIDEO: Kama ulipitwa na hii, nimekuwekea hapa sababu za Dokta Cheni kuacha kuigiza

 

Soma na hizi

Tupia Comments