Gwiji wa Liverpool Robbie Fowler amefukuzwa kazi kama meneja wa klabu ya Al Qadsiah ya Saudi Arabia, licha ya kuanza kwa ligi bila kufungwa.
Al Qadsiah wanashika nafasi ya pili katika Ligi Daraja la Kwanza la Saudi, baada ya Fowler kusimamia ushindi mara sita na sare mbili katika mechi nane za ligi.
Kufuatia tangazo la kuondoka kwa Fowler, mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na Uhispania Michel alithibitishwa mara moja kuwa meneja mpya wa klabu hiyo.
“Al Qadsiah inasitisha uhusiano wake wa kimkataba na kocha Robbie Fowler,” klabu hiyo ilisema kwenye mtandao wa kijamii.
“Tunamshukuru kocha kwa kile alichotoa katika kipindi cha mkataba na timu.”
Mshambulizi huyo wa zamani wa Reds na Uingereza, 48, amewahi kuwa kocha wa East Bengal FC katika Ligi Kuu ya India na vile vile nchini Thailand na Brisbane Roar ya Australia.