Michezo

Robinho anatakiwa kutumikia kifungo gerezani

on

Staa wa zamani wa Real Madrid na Man City Robinho (37) anatakiwa kuanza kutumikia adhabu yake ya kifungo cha miaka 9 gerezani kwa kosa la kubaka baada Mahakama ya Rufaa nchini Italia kuitupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Robinho.

Robinho raia wa Brazil alikutwa na hatia ya kosa hilo 2017 lakini kosa hilo alitenda 2013 akiwa Milan Italia sambamba na Wabrazil wenzake wengine watano ambao wanadaiwa kufanya shambulio la ngono kwa mwanamke wa miaka 22 raia wa Albania.

Kutokana na kushindwa rufaa hiyo Robinho anatakiwa kuanza kutumikia adhabu hiyo mara moja ila kwakuwa anaishi kwao Brazil kwa sasa Italy wanaweza kuomba atumikie adhabu hiyo akiwa nchini kwao Brazil

Soma na hizi

Tupia Comments