Michezo

Robinho asaini kwa mshahara wa Tsh laki 6 kwa mwezi

on

Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na Man City Robinho ,36, amerejea kwao Brazil katika club ya Santos iliyomlea na kumtoa 2002-2005 na kwenda kuanza maisha Real Madrid.

Robinho anajiunga na club hiyo kama mchezaji huru kwa mkataba wa miezi mitano baada ya kumaliza mkataba na club ya Istanbul Başakşehir ya Uturuki na sasa atacheza Santos hadi February 21 2021 kwa mshahara wa euro 230 kwa mwezi (Tsh 630,271) ukiwa ni kima cha chini zaidi ya kawaida ya kiwango cha mshahara wa wachezaji Brazil.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Robinho wakati yupo Real Madrid alikuwa akilipwa mshahara wa euro 43,750 (Tsh milioni 119.8) kwa wiki, bado haijawekwa wazi lengo la Robinho kukubali mshahara mdogo zaidi Santos.

Soma na hizi

Tupia Comments