Duniani

Teknolojia mpya iliyogundulika kufanya upasuaji wa kichwa

on

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Utah nchini Marekani wamevumbua teknolojia mpya ya Robot ambayo itatumika kufanya upasuaji ifikapo mwaka 2019 ambapo inategemewa kufanya upasuaji kwa haraka zaidi kuliko daktari wa kibinadamu.

Kwa mujibu wa daktari bingwa wa upasuaji William Couldwell, Robot hii ina uwezo wa kufanya upasuaji kwa usafi na ufanisi mara 50 zaidi ya binadamu wa kawaida ambapo itasaidia kuokoa vifo vinavyosababishwa na makosa ya kibinadamu kama vile kusahau vifaa vya upasuaji kwenye mwili wa mgonjwa.

Robot hii inatarajia kuanza rasmi kutumika kufanya upasuaji wa kichwa baada ya miaka miwili ijayo ambapo itaweza kugundua tatizo la mgonjwa kupitia machine ya CT Scan na inaweza kujizima iwapo itaona imesogea karibu zaidi na ubongo. Mashine hii itagharimu Dollar 100,000.

VIDEO: Ulipitwa na hii stori kuhusu Mtanzania aliyechora michoro ya Ikulu? Bonyeza play kutazama.

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments