Rodrygo Goes agoma kuondoka Real Madrid,licha taarifa za kuwasili kwa Kylian Mbappé majira ya joto kuwa kunatishia kupunguza muda wake wa kucheza.
Rodrygo, 23, aliifungia Madrid mara mbili katika ushindi wa 2-0 wa LaLiga dhidi ya Athletic Club Jumapili.
Kulingana na Cadena SER, kuna hamu ya mshambuliaji huyo wa Brazil kutoka vilabu vinne vya Ligi Kuu Manchester City, Manchester United, Liverpool na Arsenal pamoja na Paris Saint-Germain.
Hata hivyo, Rodrygo angependelea kusalia Santiago Bernabeu, akitazama uwezekano wa kusajiliwa kwa Mbappé kama uthibitisho kwamba Madrid wana mradi wa michezo unaosisimua zaidi katika soka la dunia hivi sasa.
Marca inakubali, ikiandika kwamba Rodrygo anataka “kusalia na kufanikiwa katika kilabu” bila “mashaka” juu ya mustakabali wake, akiwa na au bila Mbappé.