Roketi ya Starship ya kampuni ya Marekani ya SpaceX ilipiga hatua kubwa katika safari yake ya tatu ya majaribio siku ya Alhamisi, na kufikia mengi ya malengo yake.
Chombo hicho chenye sehemu mbili kilisafiri vyema kutoka kwa kituo chake cha cha kurukia huko Texas, kutuma sehemu yake ya juu kote ulimwenguni kuungana tena juu ya Bahari ya Hindi.
Mawasiliano ya redio yalipotea mwishoni mwa safari lakini kampuni hiyo ilisema “ni ajabu kuona jinsi tulivyofikia wakati huu”.
Mkuu wa SpaceX Elon Musk alifurahishwa na matokeo ya safari roketi hiyo.
Wakati chomo hicho cha urefu wa m 120 (futi 395) ilipozinduliwa mwezi Aprili na Novemba mwaka jana, ililipuka muda mfupi baada ya kuanza safari.